Muhtasari:
Programu ya Nishati Safi za Kupikia (CookFund) , inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), ni mpango wa miaka mitatu (2022 - 2024) unaolenga kuharakisha upatikanaji wa nishati na vifaa bora vya kupikia Tanzania Bara, ukilenga mikoa mitano ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma na Mwanza. Mpango huo unatekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO). UNCDF ni Meneja wa Mfuko na mtekelezaji wa Mpango.
Lugha ya pendekezo na sarafu: Andiko na Mapendekezo ya biashara yanapaswa kuwasilishwa kwa lugha ya Kiingereza. Taarifa za kifedha zinapaswa kuwasilishwa kwa kutumia TZS au Euro. Endapo kutatokea mkanganyiko wa tafsiri, tangazo la lugha ya kiingereza linachukuliwa kuwa tangazo la msingi.
Muda na Tarehe ya mwisho ya Uwasilishaji: Maombi ya awamu ya kwanza andiko la ufadhili wa mradi wa CookFund yatafunguliwa mnamo 1 Septemba 2022 na kubaki wazi hadi 16 Disemba 2022. Tathmini na mapitio ya maombi itafanywa kwa kila ombi lililowasilishwa hadi mwisho wa awamu ya kwanza. Duru za ziada za maombi mengine zitatangazwa kwa vipindi tofauti ndani ya miaka 3 ya utekelezaji wa programu ya nishati safi ya kupikia.
Jambo Muhimu la Kuzingatia: Mara baada ya kuwasilishwa, maombi yatachukuliwa kuwa ya mwisho na hayawezi kurekebishwa kabla ya mapitio na upembuzi wa awali na maoni ya UNCDF. Waombaji wasiokidhi vigezo kwa awamu ya kwanza watapata fursa ya kuelekezwa na kurekebisha kasoro zilizojitokeza ili waweze kuwasilisha maombi yaliyorekebishwa
Kwa habari zaidi na / au maswali, tafadhali wasiliana na: UNCDF Tanzania, barua pepe: cookfund.tz@uncdf.org Tel: +255 22 260 0911